Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe

Jumapili , 24th Jan , 2021

Serikali imepiga marufuku wananchi wa Kanda ya Ziwa kula nyama ya Nguruwe ikiwa ni hatua za kukabiliana na mlipuko wa homa ya nguruwe uliotokea hivi karibuni.

Picha ya mnyama Nguruwe.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dodoma Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema taarifa zilizopo zinaonyesha Homa ya Nguruwe ilianzia kwenye Halmashauri sita  za Kanda ya Ziwa.

Aidha, imewaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu karantini zilizowekwa kwa ajili ya kutibu nguruwe ambao tayari wameathirika na ugonjwa huo.

Kutokana na uwepo wa Homa ya Nguruwe tumewataka wananchi wa kanda ya ziwa kuacha kula nyama ya nguruwe ilikukabiliana na ugonjwa huu hatari ambao hauna tiba wala kinga, nawaagiza viongozi mnaohusika mikoani na wilayani kuhakikisha mnasiamia karantini zilizowekwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hausambai kwenda maeneo mengine na kuleta madhara,”amesema Waziri Ndaki.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki.

Waziri Ndaki amezitaja halmashauri ambazo hazitaruhusiwa kula nyama ya Nguruwe  kuwa ni Mbogwe, Sengerema, Geita, Misungwi, Kyerwa na Kahama ambazo kwa kiasi kikubwa zimeathirika na ugonjwa huo.

Amesema hadi kufikia Januari 22, 2020 zaidi ya nguruwe 1,500 sawa na asilimia 10 ya nguruwe wote nchini wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Mifugo Prof. Ezron Nonga amesema lengo la kuzuia wananchi kula nyama ya nguruwe ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni kudhibiti usienee kwa kasi katika maeneo mengine ambayo bado hayajaathirika.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe