Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Spika wa Bunge aagiza Lissu kurejea nchini

Jumapili , 20th Jan , 2019

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu kurejea nyumbani kwa kuwa hana kibali cha kuwa nje ya nchi.

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu.

Ndugai amesema kuwa hawezi kumpangia Lissu mambo ya kusema ila ajue hana kibali cha kuendelea kuwa nje ya nchi wakati ofisi ya Spika haina taarifa.

Yeye ametoka kuugua aache uzushi arudi nyumbani, tunamsubiri nyumbani, kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura, sasa achunge kidogo, maana Spika ana nguvu zake, asimpe sababu", amesema Ndugai.

Lissu ambaye amepona majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mwaka juzi, amedai kigezo kinachotaka kutumika kumvua ubunge ni utoro bungeni, ametoa waraka aliouita 'Baada ya risasi kushindwa, sasa wanataka kunivua Ubunge’.

Lissu ameandika katika waraka huo kuwa, “Ni taarifa gani ya maandishi watu hawa wanahitaji wakati nilishambuliwa nikiwa kwenye vikao vya Bunge Dodoma. Wakati wote ambao nimekuwa kwenye matibabu uongozi wa Bunge umewasiliana kwa maandishi na mwakilishi wa familia yangu kuhusu matibabu yangu. Wametoa matamko mengi hadharani kuhusu kushambuliwa kwangu na kuhusu matibabu yangu”.

Lissu, ambaye amemaliza matibabu yake nchini Ubelgiji na sasa anafanya ziara katika nchi za Ulaya amedai kuwa kuna mkakati wa kumvua ubunge akidai Bunge nalo linashiriki katika mpango huo.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava