Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ubaguzi wa rangi ulivyomuondoa Hector Peterson

Ijumaa , 23rd Feb , 2018

Watu wengi wanafahamu siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa Juni 16 kila mwaka, baadhi wamekuwa wakifahamu historia ya siku hii na baadhi wakiwa bado gizani ni kitu gani hasa kilisababisha kuwekwa kwa siku hii kubwa kwa kizazi cha Afrika.

Leo nakuelezea historia ya mtoto Hector Peterson, mtoto ambaye aliuawa kikatili na serikali ya makaburu nchini Afrika Kusini kutokana na ubaguzi wa rangi ambao ulikuwa umeshamiri kwa wakati huo, kwenye tukio la 'Soweto upraising', ambao lilisababisha mamia ya watu wakiwemo wanafunzi kuuawa kikatili.

Hector alizaliwa Agosti 19, 1963 na alikuwa mwanafunzi wa Junior Secondary School nchini Afrika Kusini. Siku ya tarehe 16 Juni, 1976, wanafunzi wa shule mbali mbali walikusanyika katika uwanja wa Orlando kwa ajili ya kupinga mfumo wa elimu ambao ulikuwa ni wa kibaguzi na wa kigeni ambao uko tofauti na tamaduni na lugha yao, hususan kupinga lugha ya Africaans iliyokuwa ikitumika na Kingereza kwenye masomo yao.

Walipokuwa wakitoka kwenye uwanja wa Orlando kwa maandamano ambayo yanaelezwa yalikuwa ya amani, walikutana na kundi la maaskari wakiwasubiri na kuanza kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi, wanafunzi wakaanza kuhamaki na kuanza kurusha mawe na kila walichonacho kujihami.

Askari walianza kutumia risasi za moto kuwafyatulia, na ndipo ikampata mwanafunzi Hector Peterson, alipopigwa risasi na kuanguka chini, alikuja kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mbuyisa Makhubo na kumbeba mikononi huku akikimbia naye, pembeni akiwa na dada wa Hector  Antoinette , walimchukua Hector mpaka kwenye gari ya muandishi wa habari ambaye alikuwepo eneo la tukio, na kumkimbiza kituo cha afya cha karibu lakini hawakufanikiwa kuokoa uhai wake na kufariki.

Baada ya kufariki Mbuyisa na Antoinette walipata vitisho sana kutoka kwa polisi na kulazimika kukimbia kujificha, huku Mbuyisa akikimbia nchi kabisa na hakurudi Afrika Kusini mpaka sasa, na haijulikani kama alifariki au yuko hai, tangu mama yake asema alipokea barua mwaka 1978 ya mtoto wake akisema yupo Nigeria.

Licha ya kifo cha Hector, mtoto mwengine Hastings Ndlovu ndiye alikuwa wa kwanza kupigwa risasi na kuuawa, lakini taarifa yake haikupatikana kwa haraka kutokana na kutokuwapo kwa mwandishi wa habari eneo ambalo alikuwepo.

Picha ya Hector akiwa mikononi mwa Mbuyisa na pembeni akiwepo dada yake Antoinette, ilipigwa na mpiga picha Sam Nzima, picha ambayo baada ya kuwa published ilikuwa 'icon' ya tukio la siku hiyo na dunia nzima kujua nini kinaendelea Afrika Kusini, na viongozi wengine kuanza kuingilia kati vitendo vya kibaguzi na uonevu. Pia picha hii ilimfanya Sam awe anaishi kwa kujificha kwa kuhofia kuuawa kutokana na vitisho alivyokuwa akivipata.

Baada ya Afrika Kusini kutwaa nchi yao kutoka kwa makaburu na kujitawala wenyewe na kufanikiwa kuondoa vitendo vya ubaguzi wa rangi, serikali ilijenga makumbusho maalum karibu na eneo alilouawa na kuita 'The Hector Pieterson Memorial and Museum”, ili kuenzi watoto wote waliouawa kwenye Soweto Upraising na vitendo vya ubaguzi wa rangi.

HABARI ZAIDI

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji