Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ujerumani na Tanzania kulinda Bahari ya Hindi

Jumamosi , 14th Mei , 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amekutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kufanya mazungumzo

Mazungumzo hayo yamelenga kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kwenye uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na Maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

Akizungumza jana (13.05.2022) mara baada ya kukutana na ujumbe huo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam, Dkt. Tamatamah amesema katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kutakuwa na miradi mingi ambapo kwa kuanziza Mwezi Agosti Mwaka huu 2022, mradi utafanyika Kaskazini mwa Tanzania katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kwale Mkoani Kenya.

Katibu mkuu huyo mara baada ya kukutana na ujumbe huo ambao ni Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema Tanzania itapata Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2 kwenye mradi huo katika kipindi cha miaka minne.

“Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na tunategemea mradi utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na utaongeza kipato kwa wananchi, kwa kuwa wataelimishwa njia mbadala za maisha na kuhifadhi Maeneo Tengefu.” Amesema Dkt. Tamatamah.

Naye Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema ana furaha kwamba ushirikiano wa Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na Maeneo Tengefu utakuwa na nguvu katika kuhakikisha Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi unatunzwa pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika Maeneo Tengefu zinaendelezwa, huku Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, amesema mradi huo utajenga uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Ujerumani.

Mazungumzo hayo baina ya Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann pamoja na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Bw. Ralf Senzel, yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. John Komakoma ambapo mradi huo utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Bw. Nichrous Mlalila.
 

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji