Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wabunge waungana kuaga mwili wa Dkt. Macha

Ijumaa , 21st Apr , 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dkt Elly Macha wakati wa kuaga Bungeni Mjini Dodoma leo

Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.

Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.

Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.

Dkt. Elly Macha enzi za uhai wake

Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.

Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.

Naibu Spika Dkt Tulia akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dkt Elly Macha wakati wakuaga Bungeni Mjini Dodoma leo

 

 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto