Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wakulima wapewa bilioni 164.9 na serikali

Jumanne , 31st Jan , 2023

Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mkopo wa shillingi billioni 164.9 kwa sekta ya benki na taasisi za fedha nchini uliowanufausha wakulima wadogo 5,385 na Vyama vya Ushirika na Masoko (AMCOS) 21.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Halima Mdee aliyetaka kujua makundi yaliyonufaika na mkopo wa shilingi trilioni moja iliyoahidiwa kutolewa na Serikali katika sekta ya kilimo pamoja na masharti yake.

Dkt Nchemba amesema utoaji wa mkopo huo ambao takwimu zake zinaishia tarehe 31 Desemba 2022, ulikuwa ni utekelezaji wa hatua za ziada za kisera zilizochukuliwa na serikali ikiwemo kuanzisha mkopo maalum wa shilingi trilioni moja kwa benki na taasisi za fedha nchini ili kuchochea mikopo nafuu kwa Sekta Binafsi hususan Sekta ya Kilimo.

Alisema Masharti ya mkopo huo maalum yalikuwa kuchochea mnyororo wa thamani katika kilimo cha mazao, miundombinu ya umwagiliaji, mifugo, uvuvi na ununuzi na usindikaji wa mazao yake kwa wakulima wadogo na wa kati pamoja na kampuni ndogo ndogo na za kati (SMEs).

“Masharti mengine ni Benki Kuu kuzikopesha benki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia tatu, ili taasisi hizo ziwakopeshe wakulima na kampuni zinazojishughulisha na mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10”, amefafanua Mhe. Nchemba.

Aidha, amebainisha kuwa benki na taasisi za fedha zinatakiwa kutoa mkopo usiozidi shilingi bilioni moja kwa kila mkulima kwa riba ya chini ya asilimia 10.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava