Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wale wapenda Vigodoro waambiwa kujitafakari

Jumapili , 1st Dec , 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amezitaka jamii zinazoendekeza mila na desturi, zinazochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, zikiwemo Vigodoro na Chagulaga kujitafakari.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,

Waziri Mhagama ameyabainisha hayo leo Desemba 1, 2019, Jijini Mwanza, alipozungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, ambapo amewaomba wadau mbalimbali kuangalia namna ya kuzibadilisha mila hizo ili kuweza kusaidia juhudi za Serikali, katika mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi na Virusi vyenyewe.

"Yako makabila yana Mila za chagulaga, Nyumba Ntobo, kutakasa wajane, kusafisha ghala pamoja na vigodoro ninyi muendelee kujitafakari, hizi mila zote hazituokoi, hazitupelekei kupambana na mambukizi mapya, bali zinatusababisha kuongeza maambukizi mapya na kupelekea  juhudi za Serikali kuendelea kupata changamoto", amesema Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi hapa nchini (TACAIDS), Dkt Leonard Maboko, amesema kuwa hadi kufikia leo asubuhi katika viwanja vya Rock City, jumla ya asilimia 6.3 ya waliopimwa Ukimwi, waligundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo, wanawake wakiwa 133 na wanaume 9 kati ya watu 2,265, waliojitokeza kuanzia Novemba 25.
 

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu