Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wananchi wapiga kura kumkataa mwenyekiti wao

Ijumaa , 9th Dec , 2022

Wananchi wa Kitongoji cha Rutozo kilichopo kata ya Katoro mkoani Geita wamemuondoa madarakani aliyekuwa mwenyekiti wao Joseph Mbishi kwa tuhuma za kuwakamata wanawake na kukaa nao muda mrefu ili wakombolewe na waume zao kwa kigezo cha kukusanya michango ya ujenzi wa shule

Mwenyekiti huyo ametolewa kwenye nafasi yake kwa kura za siri zilizopigwa na wananchi baada ya kushindwa kuhudhuria mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kujibu hoja za tuhuma zinazomkabili

"Waliomkubali mzee Mbishi aendelee kuwa mwenyekiti wa kitongoji ni 18, Kura zilizoharibika ni kura nane, kura zilizosema kwamba hapana kwamba asiendelee kuwa mwenyekiti wa kitongoji hiki ni kura 456, kwa mujibu wa utaratibu mzee Mbishi tutamuweka pembeni na tutapata mtu mwingine ambae atateuliwa na ofisi ya kata kwa ajili ya kuja kusimamia shughuli za maendeleo katika kitongoji hiki", alisema Shabani. 

Afisa mtendaji kata ya Katoro Selemani Mahushi anasema mwenyekiti huyo alikuwa anatuhumiwa kwa hoja nne ikiwemo kuuza viwanja vya serikali bila utaratibu maalum.

"Kutumia mtu anaejiita Afisa mazingira kufanya utapeli wa fedha kwa mwamvuli wa kuhamasisha usafi, kukusanya mchango wa ujenzi wa shule kwa kuwakamata wanawake na kukaa nao muda mrefu ili wakombolewe na waume zao na pia kuchukua vitu kama nguo na radio, kushindwa kumaliza mradi  wa ujenzi wa shule mpya Mikakati uliochukua zaidi ya miaka mitatu na wananchi kuona mradi huo unahujumiwa ",aisema Mahushi.

Baada ya zoezi la kumuondoa mwenyekiti kufanikiwa wanannchi wakalazimika kuteua watu watatu ambapo mmojawapo atateuliwa na uongozi wa kata kushikilia nafasi ya uenyekiti wa kitongoji hiko na hapa baadhi ya wananchi wanaelezea sababu za kupinga maamuzi hayo.

"Sababu Rushwa ni nyingi, kuna mtu ambao kwamba , watu watatu wale atakubalika mtu huyu mmoja, lakini yule watakaemkubali nzengo inamkubali hawatamchukua, wataenda kupendekeza kwa yule ambao watamtaka wenyewe, lakini nzengo watakaomtaka hawatakubali na sisi hili hatuwezi, sisi ndio tunatakiwa tukubaliane tuchague wenyewe si watu wale wa mbele", alisema Damas.

"Tunaomba serikali yenye mamlaka iliyoko juu kuanzia mheshimiwa  mkuu wa wilaya na mheshimiwa mkuu wa mkoa watusaidie changamoto hii tuliyonayo Rutozo tunasumbuliwa na siasa, sisi wananchi tumekubali kwa ujumla leo bila siasa yeyote  Ile tukaamua kwamba tunemtoa huyu members tupate kiongozi mwingine ambae ataendana na wananchi",  alisema Nyamhanga.

"Utaratibu wa kupata mwenyekiti wa kitongoji ni kwa mujibu wa sheria maana yake sheria, zinaelekeza kwamba baada ya kutokea hiyo hali uchaguzi kwa baadaena kwa nafasi ya serikali utatangaza na baadae kupata mwenyekiti ambae atakuwa na dhamana ya wananchi lakini kwa sasa kazi iliyopo ni kupata kaimu ambae atasimamia shughuli za maendeleo na swala Zima la ulinzi", alisema Sweya.
 

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu