Inaelezwa kuwa wagonjwa haohupelekwa katika hospitali binafsi kwa lengo la kuwapatia matibabu kwa kuwatoza fedha
Hilo limebainika mara baada ya mkurugenzi huyo kubaini kutokuwepo kwa mgonjwa wa ajali ambae alikuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mnazi mmoja katika harakati za kumtafuta mgonjwa huyo alibainika kuwepo katika hospitali ya Aasiahh S Hospitali ilipo shehia ya mkele mkoa mjini magharibi
Aidha Dr Muhidini amesema kufanya hivyo kwa madaktar hao ni kurudisha nyuma juhudi za serikali kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika sekta ya afya ili kuhakikisha wanachi wanapatiwa matibabu huku akibainisha kua wahusika wote watachukuliwa hatua za kisheria