Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Watalii wameongezeka nchini - Majaliwa

Jumatano , 5th Oct , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa watalii wanaokuja nchini Tanzania wameongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 na kufikia watalii 922,692 mwaka 2021.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Naibu Waziri Mkuu wa Mauritius kwenda kwenye ukumbi wa mikutano wa Gran Melia jijini Arusha kufungua Mkutano wa 65 wa Shirika Utalii Duniani - Kamisheni ya Afrika kwa naiba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan , Oktoba 5, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Majaliwa amesema mbali na kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini, pia mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani - Kamisheni ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha.

“Pia takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Sekta ya Utalii inazidi kuimarika zaidi hususan baada ya uzinduzi wa Programu Maalumu iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais Samia ya The Roya Tour iliyozinduliwa rasmi Aprili 2022 katika soko letu la utalii la kimkakati nchini Marekani.”

Amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mwongozo mzuri uliotolewa na Shirika la Utalii Duniani kwa nchi wanachama ikiwemo Tanzania katika kukabiliana na athari za UVIKO - 19. “Kwa msingi huo, ninatumia fursa hii kulishukuru Shirika la Utalii Duniani hususan, kwako Mheshimiwa Zurab Pololikashvili, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani kwa kuiongoza vema sekta ya utalii katika kipindi chote cha janga hilo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuendelea kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini hadi kufikia watalii milioni tano na mapato ya Dola za Marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.”Utajiri wa vivutio vya utalii tulivyonavyo umeifanya sekta ya utalii kuwa muhimili muhimu wa uchumi wa nchi yetu.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa mashirika na taasisi za kimataifa kuendelea kuiamini Tanzania na kuichagua kama sehemu sahihi ya kufanyia shughuli mbalimbali ikiwemo mikutano adhimu kama hii.

Naye, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani, Zurab Pololikashvili amesema kuwa baada ya mlipuko wa janga la UVIKO 19 nchi nyingi duniani ziliathirika kwa kiasi kikubwa katika sekta ya utalii, hivyo watahakikisha wanaendelea kuweka mikakati ya kurejesha sekta hiyo katika hali yake ya kawaida.

“Wiki iliyopita tulisherehekea siku ya utalii duniani iliyokuwa na kaulimbiu ya Rethinking Tourism, ambayo tunaamini itasaidia kuirejesha sekta hiyo katika hali yake ya kawaida na kuendelea kusaidia kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi na kuongeza idadi ya ajira.”

Amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zina vivutio bora vya kutembelea kwa ajili ya utalii na watu wengi duniani wameitambua kupitia filamu maarufu ya The Royal Tour. “Ninafurahi sana kuwa miongoni mwa watu walioshuhudia filamu hiyo ambayo imeniwezesha kuona tamaduni na vivutio vilivyopo katika ardhi hii ya Uhuru na Umoja.”

Awali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana alisema kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya nchi yetu pamoja na jumuiya ya Kimataifa katika masuala mbalimbali yakiwemo ya utalii. Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki kutoka nchi 33 wanachama wa Shirika la Utalii Duniani - Kamisheni ya Afrika.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine