Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waziri Mabula aagiza upembuzi wa mashauri ya ardhi

Alhamisi , 6th Oct , 2022

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ufanyike upembuzi wa mashauri yote ya ardhi yaliyokaa muda mrefu kutokana na sababu zisizo na mashiko.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili Kulia) pamoja na Katibu Mkuu Dkt Allan Kijazi (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara wakiwasili kwenye kikao kazi baina ya Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 6, 2022.

Amemtaka Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo kusimamia agizo hilo kwa kumpatia taarifa mapema mwezi Novemba 2022

Aidha, alimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuangalia kwa jicho la tatu Mabaraza yote ya Ardhi ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya mlundikanao wa kesi za muda mrefu.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo Oktoba 6, 2022 wakati wa Kikao kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt Mabula alisema, serikali inatambua umuhimu na michango ya mawakili katika kuvisaidia vyombo vya utoaji haki na kuwakumbusha mawakili suala la maadili ya kiutendaj hasa kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uzoefu unaonesha mashauri mengi yanayowakilishwa na mawakili ndiyo yenye kuchukua muda mrefu kumalizika.

"Mshauri mengi ya ardhi katika mabaraza hayapewi kipaumbele na Wakili anaweza kupanga tarehe ya kesi ambayo kwa siku hiyo ana mashauri katika vyombo vingine vya kutoa haki"

Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha pia baadhi ya mapingamizi yana dhamira ya kupoteza muda hususan yale mashauri yanayohusu taasisi za fedha.

"Mashauri mengi yanayofunguliwa na wananchi walioshindwa kurejesha mikopo  kwa wakati au kukiuka mikataba ya mikopo, wananchi wanakimbilia kwenye mabaraza kwa kushauriwa na mawakili". Alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ucheleweshaji mashauri kwa sababu zozote zile ni kuchelewesha kupata haki kwa wakati na kutoa rai kwa mawakili kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutumia nafasi zao kama maafisa wa mahakama kwa nia ya kuhakikisha mashauri ya ardhi yanamalizika kwa wakati na kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema, wizara yake imeitisha kikao cha pamoja na mawakili wa kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha mashauri ya ardhi katika mabaraza yanasikilizwa na kumalizwa kwa wakati.

"Mawakili wa kujitegemea mnapotekeleza kwa uadilifu uaminifu na weledi jukumu lenu la kuwakilisha wananchi katika mashauri mnawarahisishia wenyeviti wa mabaraza ya ardhi kazi ya kusikiliza na kutoa maamuzi kwa wakati kwani uwakilishi wenu kwa namna moja ama nyingine unatoa dira mapema ya kufahamu mwananchi yupi ana haki na yupi hana haki katika shauri husika" alisema Dkt Kijazi.

Kikao Kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kina lengo la kupata uelewa wa pamoja, kupokea changamoto wanazokutana nazo katika mabarza ya ardhi pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na TLS katika kutatua kero za wananchi nwenye mashauri ya ardhi.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava