Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Zitto afika kimataifa Sakata la CAG na Spika

Alhamisi , 10th Jan , 2019

Baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kwenda kuhojiwa kwenye Kamati Maadili, Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT, Zitto Kabwe ameamua kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Akbar Khan akimtaka kuingilia kati.

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Prof. Mussa Assad (kushoto), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.

Katika barua hiyo, ambayo Zitto amewatumia pia maspika wote wa nchi wanachama wa CPA na wanasheria wakuu, amesema sakata hilo lilianza baada ya Prof. Mussa Assad kusema anaamini kuwa kutotekelezwa kwa ripoti anazozitoa ni kutokana na udhaifu wa Bunge.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, amesema maoni hayo yamemfanya Spika Ndugai kumtaka Prof. Assad kufika mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ahojiwe na kujieleza.

“Mimi binafsi nimeguswa na suala hili. Naomba mabunge ya Jumuiya ya Madola muingilie kati si tu kwa sababu agizo la Spika Ndugai linavunja Katiba bali pia ni hatari kwa mustakabali wa Jumuiya ya Madola kwa ujumla”, ameandika Zitto katika barua.

Ameeleza kwamba endapo CAG ataadhibiwa na Kamati ya Bunge kwa kutoa maoni, basi ni wazi kwamba uhuru wa Taasisi ya Juu ya Ukaguzi (SAI) utakuwa umevunjwa, kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola mwaka 2013.

Tayari barua ya Zitto imekwishapokelewa na Msaidizi wa Katib Khan, Clive Barker ambaye amemjulisha Mbunge huyo kuwa amekwishapeleka ujumbe huo kwa Katibu Mkuu.

Majibu ya Barua aliyoituma Zitto Kabwe.

Spika wa Bunge Job Ndugai alimtaka CAG Assad afike kwenye Kamati ya Maadili Januari 21 kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli yake ya kwamba bunge ni dhaifu, kwa madai kwamba kauli hiyo imelidhalilisha Bunge.

 

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine