Akizungumzia hilo Ben Pol amesema kuwa ameshawahi kukuta meseji za watu mbali mbali wakiwemo wasanii Shetta, Harmonize, na msanii wa Kenya Kaligraph Jones, lakini amekuwa hazitilii maanani.
“Nawaona, Shetta, Kaligraph, naona 'blue ticks' lakini sishangai kwa sababu ni msichana mrembo, na ukikaa naye kama hivi ndio unaona urembo wake”, amesema Ben Pol.
Ben Pol kwa sasa yuko kwenye mahusiano rasmi na Anerlisa baada ya kumvisha pete ya uchumba, jambo ambalo mwenyewe anasema ni kitu kikubwa kwenye maisha yake.