Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Billnass alia na watu wenye roho mbaya

Jumatatu , 16th Jul , 2018

Rapa Billnass amesema kuwa kitendo cha video ya wimbo wake mpya ya ‘Labda’ kufutwa saa chache baada ya kuiweka katika mtandaoni ni jambo lililomuumiza na kwamba bado hajamfahamu ni nani aliyefanya kitendo hicho kwenye kazi yake hiyo kwani si mara ya kwanza yeye kupata usumbufu wa aina hayo

Rapa Billnass

Akizungumza na www.eatv.tv, rapa Billnass amesema kuwa kuna mtu atakua anahusika moja kwa moja na tukio hilo la kuchezea video za nyimbo zake pindi zinapopakiwa katika mtandao wa Youtube.

“Kuna mtu atakua anahusika aidha kwa kupenda au kimakosa, japo kwa sasa kuna mtu ambaye amenirudishia video hiyo na kwa sasa ipo sawa. Mimi sio mtaalamu sana sababu huwa natumiwa ‘link’ tu pale wimbo unapokuwa tayari umepakiwa kwenye ‘Youtube’. Na yupo mtu wangu ambaye anahusika na kupakia video za nyimbo zangu katika mtandao wa youtube. Jambo hili liliwahi kunisumbua kwenye ‘link’ ya wimbo wa 'Tagi Ubavu' mpaka leo inashida na mpaka sasa bado tunajaribu kujua watu gani wanacheza nayo”, amesema Billnass.

Awali kupitia mtandao wake wa Instagram Billnas aliandika kuwa amesikitishwa na kitendo cha video yake kufutwa katika mtandao wa ‘Youtube’ ikiwa hata haijatazamwa vya kutosha na kuwalaumu watu wenye roho mbaya kuwa ndio wamefanya kitendo hicho wakati yeye huwasapoti wanamuziki wengine kwa moyo mmoja pindi wanapotoa nyimbo zao.

“Kitendo Cha video yangu ‘ku-hackiwa’ na Kufutwa Youtube kimeniumiza sana. Video Yangu hata haina umri wa masaa mengi, waliotazama wenyewe sio wa kiivyo ndio imeanza kuingia kwenye ‘trending’ watu wenye roho mbaya wamefanya wanayoweza. Sijawahi Kufanya muziki wa mashindano, mara zote huwa nasapoti kazi za wenzangu kwa moyo mmoja pia huwa natoa nyimbo kwa muda mrefu sana nikiwa naamini kila mtu ana nafasi yake na muda wake.

Nafanya muziki wangu kujikwamua na umaskini wangu na kuiendeleza karama aliyonipa Mwenyezi Mungu, sio kumkomoa mwingine. Sidhani kama roho za namna hii zinaweza kukuza tasnia. Imeniumiza sana na inatisha sana kama Muziki wetu umefikia huku”, amesema Billnass.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa