Msanii Lulu Diva na gari lake la Jeep
Akizungumza baada ya kudakwa na Kamera ya EATV & EA Radio Digital Lulu Diva amesema gari hiyo ameinunua na ina thamani ya Milioni 300 za kitanzania pia rangi yake haifanani na gari la msanii yeyote hapa Bongo.
Aidh Lulu Diva ameendelea kusema kama kuna mtu yeyote anayebishia gari lake kama amenunua kwa bei hiyo anaweza aka-google kuangalia gharama za bei hizo ili kupata uhakika.
Kwa ndinga hii inadhihirisha kuwa kwa sasa Lulu Diva ndiyo anaongoza kumiliki gari yenye thamani kuliko msanii yeyote wa kike hapa Tanzania.