Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Moyo ulivyomtesa Alikiba, Ben Pol, V Money na Jide

Jumapili , 20th Sep , 2020

Moyo ni kiungo kikubwa na muhimu sana katika mwili wa binaadam yeyote aliye hai hapa duniani na moyo huohuo ukishindwa kufanya kazi yake vizuri unaweza kupata magonjwa au kupoteza maisha kabisa.

Picha ya Moyo

Ila tuangalie moyo kwenye upande wa burudani na mahusiano kama ambavyo wasanii wengi wa BongoFleva walivyolalamika kuhusiana na hilo kwenye nyimbo zao.

Moyo mashine - Ben Pol 

Wimbo huu wa Ben Pol ulitoka mwaka 2016 ilifanya vizuri sana kwenye chati za muziki hapa Tanzania, mpaka sasa ina watazamaji Milioni 8 kwenye mtandao wa Youtube, kwenye ngoma hiyo Ben Pol ameusifu moyo wake hadi kuuita moyo mashine kwa kuvumilia, kuzungushwa, kusemwa na kutokata tamaa kutoka kwa mtu ambaye anampenda.

Usiusemee Moyo - Lady Jay Dee 

Miaka 20 ya Komando Jide ina moyo wake pia ambapo mwaka 2003 alitoa wimbo wa usiusemee moyo wa mtu kama kujigamba kwa wengine kama anakupenda sana hali ya kuwa akitoka nje hujui alitendalo, wimbo huo ulishinda tuzo ya wimbo bora wa RnB kwenye tuzo za 'Tanzania Youth Achievements Awards

Moyo wangu - Rose Muhando 

Malkia huyu wa muziki wa Injili Tanzania aliimba wimbo kuhusiana na moyo ambapo amezungumzia kuwa moyo wake atamkabidhi Yesu na sifa zote atampa Yesu Kristo.

Moyo sukuma damu - Lameck Ditto 

Alikuwa kimya kwenye game ila baada ya kuachia kazi ya moyo sukuma damu alirudi vizuri na alipokelewa vizuri kwa mashabiki wa muziki hasa wale waliotendwa kwenye mahusiano ambapo walitumia wimbo huu kama kufuta mawazo, kujiliwaza na kujipa moyo kuhusu mahusiano.

Moyo - Vanessa Mdee 

Vanessa Mdee amelalamika sana kwenye huu wimbo wa moyo, tena aliachia kazi hii baaada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake msanii Juma Jux, Vanessa anasema moyo umemkosea sana kwani alimpa mtu ambaye hukumthamini, alimsaliti na mlevi, imepita mwaka mmoja sasa tangu Vanessa Mdee kutoka wimbo huo ambao ulipendwa zaidi na kina dada.

Mali yangu na Mbio - Alikiba 

Kwenye nyimbo hizi mbili staa wa BongoFleva Alikiba aliiimba kuhusiana na moyo, kwanza kwenye wimbo wa mali yangu ambapo anasema kama alifanya makosa moyo wake kumpenda na kumchagua mwanamke ambaye alimsaliti.

Pia kwenye wimbo wa mbio akasema kupenda pasipo thamani kwa upande wake anaona sio sawa hivyo ni bora apewe moyo wake aufiche.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava