Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ndoa ya Kiba yamtoa povu Dully Sykes

Jumatatu , 16th Apr , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya , Dully Sykes, ametoa ya moyoni baada ya kutoalikwa harusi ya msanii mwenzake Alikiba, ambaye kwa asilimia kubwa amehusika kwenye sanaa yake ya muziki mpaka kufikia alipo sasa.

Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema hajapewa taarifa yoyote kutoka kwa Ali Kiba licha ya kuwa mtu wake wa karibu, zaidi ya kuona mitandaoni na kuthibitishiwa na watu wa Mombasa.

“Mimi hajaniambia chochote na wala sijui, nimeona tu mitandaoni na nimepigiwa simu na dada yangu kutoka Mombasa, amenitaarifu kwamba Ali anaenda kuoa kule, lakini Ali hajaniambia chochote, mimi ni mtu ambaye nilikuwa namsapoti na ndiye nilianza kumkubali, kipindi hiko hakuna mtu yeyote anayemjua Ali Kiba, hata nyumba ya jirani hawamjui kama msanii, na niliposikia sauti yake tu nikamuomba collabo”, amefunguka Dully Sykes.

Hata hivyo Dully Sykes amesema anamtakia Alikiba maisha mema kwenye ndoa yake, kwani ni jambo la heri na kumsihi asichukulie mzaha suala la ndoa.

“Namtakia ndoa njema, nampenda sana na anajua, namtakia maisha mema, na namsihi ndoa sio kitu kidogo, anapoamua kuchukua mtoto wa watu, hasa ambaye amemchukua nchi nyingine, inabidi amuheshimu sana, amuonyeshe upendo hata yule mtoto akiitwa na wazazi wake mbona huji kutuangalia akose cha kuwaambia kwa upendo atakaompa”, amesema Dully

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Alikiba anatarajia kuoa hivi karibuni, ndoa ambayo imetangazwa kufanyika kwa siri nchini Kenya mjini Mombasa, na mpaka sasa mwanamke anayetarajia kuolewa na Alikiba hajajulikana ni nani kwa picha.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava