Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nikki Mbishi atoa onyo kwa Nikki wa Pili

Jumanne , 30th Apr , 2019

Rapa Nikki Mbishi 'Unju' amemtaka rapa wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili kuacha kumzungumzia endapo hawezi kumuongelea kwa mazuri kuliko anavyoendelea kumchafulia taswira yake.

Nikki Mbishi na Nikki wa Pili

Nikki Mbishi amelazimika kusema hivyo ikiwa ni baada ya video kadha za mahojiano zilizomuonesha Nikki wa Pili akisema hawezi kufanya kazi na Nikki Mbishi kutokana na kwamba hawana mahusiano mazuri ya kibiashara.

"Hiki kijamaa cha kuitwa Nikki Wapili kila kikiulizwa swali kuhusu mimi lazima kiongee CHOO, as if chenyewe ndio kinafanya biashara bora ya muziki, babu ni hivi kama huwezi kufanya kazi na mimi sema huwezi sio kila siku kujaribu kushawishi watu kuwa mimi ni mtu mbaya kwenye biashara".

Ameongeza, "kama huwezi kuniongelea kwa taswira safi na chanya kwa msimamo na mtazamo wangu basi kausha sio mpaka ushawishi watu kuwa NIKKI MBISHI hafai kwanza wewe ni msemaji wa WEUSI sio wa UNJU".

Katika kauli yake Nikki wa Pili alinukuliwa akisema kwamba kwa mtazamo wake katika wimbo wa Wapoloo hawawezi kufanya remix na Nikki Mbishi kutokana na kutojali mahusiano yake na watu jambo ambalo kibiashara siyo zuri.

Akijibu kauli hiyo Nikki Mbishi amesema, "kwanza kazi zenu huwa hamshirikishi watu ishazoeleka, kwahiyo acha kuchafua jina langu. Jifunze kunyamaza kama huna lolote la kunizungumzia. Naongea na wewe Nikki Wapili maana naona tu interviews zako, oooh UNJU hana mahusiano mazuri na watu, watu au nyie tu?. Utadhani hata mshawahi kufurahi mkiona wengine wanapata nafasi. Halafu ni hivi mi sio msanii wa media ni msanii wa mitaa ambayo haifuatilii hata media wakati mwingine mnaimbia media mi narap kwa ajili ya mitaa".

Baada ya tuhuma hizo, Nikki wa Pili amemjibu Nikki Mbishi, "kitaa kuna watu wazima, watoto, wasichana, wakaka, saloon, migahawa, bajaji, boda, uber, kuna sherehe za birthdays na kadhalika, ukisema unafanya muziki wa kitaa basi upatikane huko, ujadiliwe huko uwe kwenye playlist za huko uzunguke huko hicho ndio kitaa kujidanganya ni kazi rahisi".

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu