Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Shilole ahusika kwenye 'mjengo' wa Man Fongo

Jumapili , 15th Jan , 2017

Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fong amemtaja msanii mwenzake wa bongo fleva na bongo movie, Shilole a.k.a Shishi Trump kuhusika katika ujenzi wa nyumba yake ambayo anataraji kuijenga wakati wowote kutoka sasa.

Shilole

Man Fongo aliyekuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Ujenzi cha EATV, amesema mtu pekee aliyemuhamasisha kujenga nyumba ni Shilole, na hiyo ni baada ya siku moja kutembeea nyumbani kwa Shilole na kukuta vitu ambavyo yeye aliona ni vya ajabu na kujikuta anavipenda na kutamani kuwa navyo katika nyumba yake.

Alisema jambo la kwanza alilofanya kukusanya fedha na kununu kiwanja ambacho kiko tayari na amekinunua maeneo ya Kimara Bonyokwa na muda wowote ataanza kuporomosha mjengo wake.

Amesema hawezi kumsahau Shilole kwa kumpa hasira za kuweka mjengo huo, ambao amesema ataujenga taratibu kwa kadri atakavyokuwa anapata pesa na anatamani uwe na vitu vyote vizuri kama ambavyo huwa anaviona kwa washkaji zake hasa Shilole, licha ya kuwa yeye ni mtoto wa uswahilini.

Man Fongo

"Sina nyumba, lakini nina kiwanja Kimara Bonyokwa na Shilole ndiye aliyenipa hasira ya kumiliki mjengo wangu, mimi ni mtu wa uswazi lakini kuna vitu ningependa kuviweka kwenye mjengo wangu, natamani kuwa na vitu vizuri, kama ninavyoona kwa wenzangu..... kwa mfano pale kwa Shishi nimeona amechora chora hivi kwa pembeni, halafu juu kuna madude hivi mimi huwa naita ceiling board, nyie sijui mnaitaje (Gypsum) eheee" Amesema Man Fongo.

Amewashauri vijana hususani wasanii wenye uwezo na kipato kujenga nyumba zao, kwani ni muhimu na si lazima kujenga haraka bali kwa utaratibu kadri watakavyokuwa wakipata pesa.

"Kama mimi ndo nimeanza kupata kipato changu kidogo, nimeanza kununua kiwanja... kujenga hakuhitaji papara, kama leo ukishindwa, zamu yako itakuja kesho" Alimalizia Man Fongo

 

 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava