Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Shule 9 za Mtwara zilizopatiwa taulo za kike

Jumatano , 5th Oct , 2022

Mwezi Septemba mwaka huu kampeni ya Namthamini ilianza kugawa taulo za kike katika Mkoa wa Mtwara kwa lengo kuwasadia wanafunzi kubaki mashuleni kwa mwaka mzima na kupunguza changamoto wanazopata katika kipindi cha hedhi.

Mtangazaji wa East Africa TV, Najma Paul akifurahi na wanafunzi wa Masasi baada ya kumaliza kugawa taulo za kike katika shule hiyo.

Septemba 19 kampeni ya Namthamini ilianza katika Wilaya ya Mtwara kwa kugawa taulo za kike katika shule ya sekondari Mikindani walioungana na wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Mitengo, ambapo jumla ya pakiti 862 za taulo za kike zilitolewa kwa wanafunzi shule hizo mbili, pamoja na kutoa elimu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike na kiume.

Pia katika siku hiyo kampeni ya Namthamini iliendelea katika shule ya Sekondari Naliendele walioungana na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Mangamba, ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 969 zilitolewa kwa wanafunzi wa shule zote mbili.

Septemba 20 kampeni ya Namthamini iliendelea katika wilaya ya Masasi ambapo ilifika katika shule tatu za sekondari nazo ni Chiungutwa, Lukuledi na Masasi ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 3048 zilitolewa kwa shule hizo tatu.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Chiungutwa walipatiwa taulo za kike pakiti 1008

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lukuledi walipatiwa taulo za kike pakiti 1056

Kampeni ya Namthamini wilaya ya Masasi ikamaliza kugawa taulo za kike katika wilaya hiyo katika shule ya Sekondari Masasi ambapo wanafunzi wa shule hiyo walipatiwa taulo za kike pakiti 984.

Septemba 21 kampeni ya Namthamini ikamaliza kugawa taulo za kike katika mkoa wa Mtwara katika wilaya ya Nanyumbu ambapo ilifika katika shule mbili za sekondari nazo ni Napacho na Nanyumbu.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Napacho ilipatiwa taulo za kike pakiti 1050.

Kampeni ya Namthamini katika mkoa wa Mtwara ikamaliza kugawa taulo za kike katika shule ya Sekondari Nanyumbu ambapo jumla ya taulo za kike pakiti 1008 zilitolewa katika shule hiyo.

Kampeni ya Namthamini itaendelea kugawa taulo za kike mwezi Oktoba katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.

HABARI ZAIDI

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji