Kupitia video moja katika mtandao wa Twitter, inaonesha wakazi mbali mbali waliokuwa njiani wakishuka kwenye magari yao na kuokota pesa hizo, kitendo ambacho kimesababisha ajali ndogo ndogo za barabarani kwa mujibu wa polisi wa kitongoji cha East Rutherford katika mji huo.
Kampuni ya magari hayo ya kubebea pesa inayojulikana kama 'Brinks', imethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, lakini wameshindwa kujua ni kiasi gani cha pesa kilichopotea.