Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Zijue athari za kubaki kwenye penzi lililoisha

Alhamisi , 19th Sep , 2019

Katika mahusiano kitu kikubwa kinachozungumziwa ni hisia na mahusiano ni uwekezaji na ukiwekeza mahali na uone haupati faida wala marejesho yoyote, ni lazima utaona imekuwa kama biashara kichaa.

Picha ya mfano wa mtu mwenye msongo wa mawazo

Kwa Mwanamke na Mwanaume kila mmoja anatarajia marejesho kutoka kwa mwingine, ikiwemo kupatiwa huduma ama kujuliwa hali lakini unakuja kushangaa kila kitu kinakuja kuwa tofatuti.

Mwanasaikolojia John Ambrose anasema kuwa kuna aina takribani tano za mahusiano, katika mahusiano hayo kuna watu ambao wanayo mahaba yaliyopitiliza, kuna wengine hawapendi kuwajibika wengi wao wakiwa wanaume kwa maana nyingine ni watu wenye dharau, Ambrose anasema ukiolewa na mtu wa aina hii lazima utaumia.

Mahusiano pia  yanategemea haiba ya mtu, kuna watu ni wapole na wanyenyekevu na hawapendi mahusiano yao yaharibike, lakini pia kuna watu wengine ambao wameathiriwa na malezi ambao hawezi kufanya maamuzi bila familia zao .

Lakini hisia ni kama 'keyboard' inayotawala mahusiano na inategemea hisia za mtu zimejengeka vipi kimazingira. Wanawake wapole na wanyenyekevu wasiopenda changamoto ndio viumbe wanaoumia zaidi katika mahusiano.

Mwanasaikolojia huyu ameitaja jinsia ya Kike ndiyo rahisi sana kubaki katika penzi lililoisha na hii inaenda zaidi kwa wanawake walio katika ndoa, ambao mara nyingi hubaki kwa kuhofia maisha ya watoto wao waliowazaa kwa kuhofia endapo akiondoka watoto hao watateseka.

Mwanasaikolojia huyo wa masuala ya mahusiano, amezitaja athari za kubaki katika mahusiano yaliyokwisha ni pamoja na vifo na watu kuuana, kuingia kwenye mahusiano ya kulazimisha.

Jambo lingine ni kuingia katika mahusiano ambayo hatujayafanyia utafiti, hali inayopelekea watu kupata  makovu ya Moyo, ugonjwa wa upweke na kupelekea kinga ya mwili kushuka na kukutwa na mafua ya mara kwa mara.

Athari nyingine ni ya uchumi na kupata Sonona kwa kushindwa kufanya shughuli zako na utendaji wa kazi kushuka na kuwa na hofu kubwa huku wengine wakiamua kujiua na kuwa wakatili .

Aidha Ambrose anatoa ushauri kwa watu ambao bado hawako katika mahusiano, kwamba mapenzi ni Sayansi hivyo ni vyema ukasoma kwanza kabla ya kuingia na malumbano yanayotokea yanatokana na jinsi ambavyo mlivyoanza na kwa upande wa watu waliokatika mahusiano anawashauri ni vyema kutunza mazuri ya mwenzako zaidi, kuliko kutunza mabaya yake.
 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava