Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Aussems ataja listi ya wachezaji aliowataka

Ijumaa , 26th Jul , 2019

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji Patrick Aussems,  amezungumzia usajili uliofanywa na klabu hiyo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya Kimataifa.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems

Aussems amesema kuwa kabla hajakwenda likizo aliacha orodha ya wachezaji nane, ambao mpaka sasa wamesajiliwa wachache kati ya hao huku akionekana kuridhishwa na viwango vya wachezaji waliosajiliwa.

Amesema, “nimefanikiwa kwa kiasi fulani mpaka sasa kuwaandaa vijana na nimeona wote wapo vizuri na wanajuhudi kubwa uwanjani. Natengeneza kikosi bora kwa ajili ya msimu ujao''.

Niliacha majina nane kabla sijaondoka kwenda likizo, baadhi wamesajiliwa akiwemo Msudan ambaye nilimuona muda mrefu na nimempenda kiukweli ila wengine bado hawajasajiliwa lakini waliopo ni wazuri sana na wanafanya kazi kwa juhudi,” amesema Aussems.

Kwa mujibu wa Simba, mpaka sasa imebakiza nafasi ya mchezaji mmoja pekee kumsajili, baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wapya akiwemo, Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Tairone da Silva hawa ni raia wa Brazili ambao wamesaini kandarasi ya miaka miwili.

Wengine ni Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman raia wa Sudan, Beno Kakolanya, Miraj Athuman, Francis Kahata, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji