Hayo yamebainishwa leo na Wakili wa serikali, Nassoro Katuga na kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika na jalada limepelekwa kwa DPP ili aweze kulipitia na kuona kama umekamilika au laa
Mara baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa ameamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo na kusikilizwa tena hadi Septemba 27 mwaka huu.
Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi michache iliyopita wakikabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha.