Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Droo ya robo fainali Afrika, inafanyika kesho

Jumatatu , 4th Apr , 2022

Droo ya michezo ya hatua ya robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho inafanyika kesho Aprili 5, 2022 makao makuu ya shirikisho la Soka Afrika CAF Cairo Misri. Droo hii itahusisha jumla ya timu 8 kwenye kila michuan, zilizofuzu kutoka hatua ya makundi.

Droo ya hatua ya robo fainali klabu bingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika inafanyika kesho

Hatua ya makundi ya michuano hii ilikamilika jana kwa michezo ya mwisho ya hatua ya makundi kuchezwa kwenye makundi yote 4 na timu mbili za juu zilizomaliza nafasi ya kwanza na ya pili kwenye kila kundi ndizo zilizofuzu hatua ya robo fainali.

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali upande wa klabu bingwa ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Club Athletic ya Morocco, Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia na Wydad Athletic Club ya Morocco hizi zimemaliza kama vinara wa makundi. Na zile zilizofuzu kama washindi wa pili kwenye makundi ni Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad, ES Setif zote za Algeria na Petro de Luanda ya Angola.

Kwenye kombe la shirikisho timu zilizofuzu kama vinara wa makundi ni Al-Ahli Sports Club ya Libya, TP Mazembe ya DR Congo, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na RS Berkane ya Morocco. Waliofuzu kama washindi wa pili ni Pyramids, al- ittihad, Al Masry na Simba sc.

Timu zilizomaliza kama vinara wa Makundi zitapangwa juu halafu zilizomaliza nafasi ya pili zitachaguliwa kucheza na vinara wa makundi katika droo ya kesho. Lakini pia vinara hao wa makundi watapata faida ya kuanzaia ugenini kwenye michezo ya mkondo wa kwanza na mchezo wa pili watamaliza katika viwanja vyao vya nyumbani.

Katika hauta hii timu zilizokuwa kundi moja haziwezi kukutana lakini zile zinazotoka kwenye nchi moja zinaweza kupangwa kucheza kwenye hatua hii.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji