Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hofu ya zidane dhidi ya Liverpool

Jumanne , 22nd Mei , 2018

Katika kuelekea mchezo wa fainali wa mashindano ya klabu bingwa Ulaya, kocha mkuu wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane amesema kitu pekee anachohofia katika mchezo huo ni washambuliaji wa Liverpool wakiongozwa na Mohamed Salah.

Kwa mujibu wa gazeti la Independent, Zidane amesema hayo leo Mei 22, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa Liverpool ni timu bora baada ya kuwa na msimu mzuri katika ligi kuu ya England na pamoja michuano ya Ulaya na timu hiyo inayostahili kuwepo katika fainali ya klabu bingwa Ulaya.

“Ninachoogopa kuhusu hii timu (Liverpool), kinachozungumziwa ni wachezaji  watatu wa mbele au mapungufu ya safu ya ulinzi, wanastahili kuwepo katika fainali kama sisi, ni wachezaji wenye ukaribu sana, jukumu letu pamoja na benchi la ufundi ni kuhakikisha tunajiandaa vya kutosha na mchezo huo kujua mapungufu ya mpinzani wetu na kuwaadhibu” amesema Zidane.

Zidane ameongeza kuwa ikitokea amepoteza mchezo huo bado haitakuwa kama ni kushindwa bali jambo pekee aliloshindwa katika msimu huu ni kutolewa katika hatua ya Robo fainali dhidi ya Leganes katika kombe la mfalme “Copa del Rey” nchini Hispania.

Jumamosi Mei 26, 2018 mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania watakabiliana na klabu ya Liverpool kutoka England katika  mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya katika Mji wa Kiev nchini Ukraine.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine