Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Manara amvaa Mwinyi Zahera kuhusu Kakolanya

Jumapili , 16th Dec , 2018

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka na kutoa maoni yake juu ya mlinda mlango wa Yanga, Beno Kakolanya ambaye amekataliwa na kocha wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera.

Haji Manara na kocha, Mwinyi Zahera

Hayo yamekuja baada ya kocha wa Yanga kuonekana katika video moja akisema kuwa klabu hiyo haina haja ya kuendelea tena na Beno Kakolanya na badala yake atafute klabu nyingine inayoweza kumsajili, baada ya kugoma kucheza kutokana na kudai maslahi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika, "nahitaji povu la omo, la foma nimpelekee Congo Meneja huyu anayetajwa hakuwepo wakati Beno alipowaokoa na 'saves' zaidi ya kumi walipopaki basi miezi michache nyuma?.  Jibu ni rahisi tu, wenzetu hubebana sana sana, hapo anatengenezewa mazingira 'papaa ndoki' aje kuwa nyanda namba one kama mnabisha muda utahukumu."

Katika video maalum wakati akiongea na mtandao wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera alisema, "kurejea Yanga, hilo haliwezekani. Kesho (jana) dirisha litafungwa, sijui saa ngapi, wale waliomwambia asiende mazoezi, kama ni mameneja wake au ni watu gani, wao ndiyo wamtafutie timu ila hapa kwetu nadhani kama haiwezekani tena."

Dirisha la usajili limefungwa saa 6:00 usiku ya Disemba 15 na hatma ya Beno Kakolanya bado haijafahamika ni wapi ataelekea. Yanga inatarajia kushuka dimbani hii leo kukipiga na Ruvu Shooting, mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utaochezwa katika uwanja wa taifa.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji