Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mashali kuwaongoza mabondia wa Tanzania kusaka UBO

Ijumaa , 13th Mei , 2016

Bondia Mtanzania Thomas Mashali ametamka wazi kuwa leo Mei 14 itakuwa siku ya kukumbukwa na Watanzania hasa wapenda michezo wa masumbwi, pale atakaoipeperusha vema bendera ya taifa akimpa kipigo kizito bondia Sajjad Mehrab wa Iran kesho.

Bondia Thomas [Mashali kushoto] akijifua na mkongwe Rashid Matumla.

Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania na mpinzani wake Sajjad Mehrab wa Iran hapo jana wamepima uzito na afya zao tayari kabisa kwa mpambano wa kimataifa wa raundi 12, kuwania ubingwa wa dunia wa UBO uzito wa juu mwepesi mpambano utakaofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Katibu mkuu wa shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania PST ambao ndiyo wasimamizi wa ndani Anthon Ruta amesema maandalizi ya mpambano huo na mengine ya utangulizi yamekamilika huku bondia Thomas Mashali ambaye alikuwa akinolewa na Mkongwe Rashid Matumla yeye akiahidi kuibeba Tanzania leo..

Aidha Ruta amesema mabondia wote wawili wametimiza vigezo vyote vya mchezo wao ambapo Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia kg 76 mkanda wa U.B.O na Sajjad Mehrab kutoka 'Irani' baada ya wote kulingana uzito na kuwa na afya njema.

Pamoja na mpambano huo mkubwa pia hiyo kesho kutakuwa na patashika nyingine kwa mapambano mengine ya kimataifa yatakayowakutanisha mabondia Mwanadada Lulu Kayage atakaezichapa na Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi na Allen Kamote atapambana na Salim Chazama wa Malawi.

Mapambano mengine ni kati ya Ramadhan Shauri atakayepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya

Na mbishi kutoka Kinondoni Fransic Miyeyusho 'chichi mawe yeye atavaana na Sajjabi Ben wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edwrd Kakembo wa Uganda hayo yakiwa ni mapigano ya kimataifa huku mapambano mengine ya kitaifa yatawakutanisha  Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola pambano ambalo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ameahidi kutoa zawadi binafsi ya vifaa vya mchezo wa ngumi kwa mshindi kati ya Nampepeche na Mazola.

Akimalizia Ruta amesema siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesha nidhamu ya mchezo wa masumbwi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua shiria za mchezo huo.

HABARI ZAIDI

Picha ya Diddy na Cassie enzi za mahusiano yake

Diddy aomba msamaha kumshambulia EX wake Cassie

Rais wa Iran Ebrahim Raisi

Rais wa Iran afariki kwa ajali ya Helikopta

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi