Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mo Dewji agawa usafiri kwa wachezaji wote wa Simba

Jumatano , 22nd Mei , 2019

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji, ametoa usafiri kwa wachezaji wote wa Simba msimu huu ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwao kutokana na mafanikio waliyopata msimu huu.

Mo Dewji na kikosi cha Simba

Akiongea leo baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi kuu kwa mara ya pili mfululizo, Mo Dewji amesema anatekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wachezaji wa Simba wanakuwa na maisha bora kwa kuwapa pikipiki aina ya Boxer zitakazowasaidia kuongeza kipato.

''Kalbu yetu msimu huu imetoa bonus kubwa sana kwa wachezaji ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni moja, na mimi binafsi nimetoa pikipiki kwa kila mchezaji, ambazo zitawasaidia kuinua vipato vyao kwani wakiweka watu wa kuziendesha zinaweza kuwaingizia 15,000/= kwa siku'' - Mo Dewji.

Aidha Mwekezaji huyo wa Simba amesema kuhusu Pre season ya msimu ujao, wamejipanga kwenda Marekani au Ureno.

''Nimeongea na viongozi wa DC United ya Marekani na nimeomba tukafanye Pre season huko pia tucheze nao na timu nyingine za LMS au kwenda Ureno tukacheze na timu za huko'', ameeleza.

Kwa upande wa usajili amesema wapo makini na leo watapata ripoti ya kocha juu ya wachezaji wa nyumbani anaowataka, lakini pia katika wachezaji 10 wa kigeni mpaka leo usiku kocha ataeleza anabaki na nani na kina nani waondoke.
 

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu