Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mwambusi amtaja aliyeiangusha Yanga

Jumapili , 26th Feb , 2017

Mara baada ya Yanga kuchezea kipigo cha mabao 2- kutoka kwa mahasimu wao Simb, Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amefunguka sababu za timu yake kupoteza mchezo mojawapo ikiwa ni kuumia kwa kiungo wake Thaban Kamusoko.

Mwambusi (Kushoto):
Kulia ni Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib akimtoka beki wa Yanga Mwinyi Haji katika mchezo huo ambao Simba imeshinda bao 2-1

Mwambusi amesema kuumia kwa Kamusoko kuliwafanya Simba waje zaidi katika eneo la katikati, jambo ambalo liliwasaidia kupitisha mipira kirahisi na hatimaye kuweza kupata mabao mawili na kuibuka na ushindi.

Amesema licha ya kumuigiza Said Makapu kuchukua nafasi ya Kamusoko, lakini hakufanya kazi ipasavyo, na pia anapungukiwa baadhi ya vitu alivyonavyo Kamusoko ikiwa ni pamoja na kuwa na maono pamoja na kuunganisha safu ya nyuma na mbele.

Sababu nyingine aliyoitaja Mwambusi ni umakini wa wachezaji wote kwenye timu yake kupungua na kushindwa kukaba, jambo lililofanya wawe wanakaba kwa macho.

"Wao Simba waliongeza namba katikati, sasa na sisi vijana wetu tuliowaingiza baada ya kamusoko kuumia walipaswa walitakiwa kuongeza namba katikati lakini wakashindwa,.... Pia umakini wa ukabaji kwa wachezaji wetu haukuwa mzuri, Simba walikuwa wanakuja wanapita watu wanawasindikiza kwa macho" - Amesema Juma Mwambusi.

Hata hivyo amesema matokeo hayo inagawa yanawaumiza, hayajawapotezea lengo lao la kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania na kwamba atakaa na walimu wenzake kurekebisha makosa ambayo yamejitokeza ili yasijirudie tena.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mavugo na Kichuya kipindi cha pili, huku la Yanga likifungwa na Msuva kwa njia ya penati, katika dakika ya 5

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu