Mesut Ozil
Dili la sasa la mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani klabuni hapo linamalizika katika msimu ujao wa joto na kumekuwa na ripoti zinazodai kwamba Mjerumani huyo ataondoka Arsenal katika kapindi hicho.
Pamoja na tetesi hizo kuhusu kuachana na Arsenal, Ozil mwenyewe amesema hana mpango wowote wa kuondoka na kwamba ametulia kwenye klabu hiyo, huku akiamini kuwa wataanza kucheza vizuri baada ya kipindi kibaya cha hivi karibuni ambacho kimeipa wakati mgumu timu hiyo kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa kuwa nje ya timu nne za juu kwenye msimamo wa EPL