Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Robetinho aiwaza fainali ya CAF

Jumanne , 3rd Jan , 2023

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Robertinho Oliviera ‘Robertinho’ amesema siku zote anawaza vitu vikubwa na malengo yake ni makubwa ikiwemo kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robertinho ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu na  amesema watu wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu hatua ya makundi lakini ukiweka mipango mizuri hata fainali inawezekana.

Kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu, Robertinho amesema yeye ni mshindani na anaamini katika mipango dhabiti hivyo kila kitu kinawezekana.

“Nimewahi kuwa mchezaji kabla ya kuwa kocha, siku zote naamini katika mipango mizuri. Ukiwa na mipango mizuri unaweza kufika nusu fainali mpaka fainali hilo linawezekana pia nikiwa hapa Simba.

“Wakati niko Vipers tulipokuwa tunaenda kukutana na TP Mazembe wengi waliamini ulikuwa mwisho wetu lakini tulikuwa na mipango mizuri mpaka tukafanikiwa kuwatoa,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu amesema kitu kilichotuvutia kwa Robertinho ni ubora na uzoefu wake kwa soka la Afrika Mashariki kwa hiyo tunaamini atatufikisha tunapopataka.

“Robertinho ni kocha mwenye wasifu mkubwa nasi tuna malengo makubwa ndiyo maana tumemchukua, ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika Mashariki hilo pia limetuvutia,” amesema Mangungu.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava