Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serengeti Boys kuvaana na Marekani na Korea Kusini

Jumanne , 19th Apr , 2016

Timu ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania waliochini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imeendelea kupata neema baada ya kucheza na wenzao wa Misri sasa wamepaata mwaliko kwenda nchini India kushiriki michuano maalumu ya nchi tano duniani.

Mchezaji wa Serengeti Boys akiwatoka wachezaji wa Misri wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni nchini

Timu ya taifa ya Tanzania vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kushiriki mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India, yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia na Korea Kusini na wenyeji mapema mwezi Mei, 2016.

Chama cha Soka cha India (AIFF) kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Jumla ya nchi tano zitashiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika mji wa Goa kuanzia Mei 15-25, 2016, ambapo michezo itachezwa kwa mfumo wa ligi kwa kila timu kucheza michezo minne, kabla ya mchezo wa mwisho wa fainali wa kumpata bingwa wa mashiandano hayo.

Serengeti Boys ambayo imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa mpaka sasa, mmoja dhidi ya Burundi na miwili dhidi ya timu ya vijana wa Misri (The Pharaohs) inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa kwa safari ya kuelekea nchini India kushiriki michuano hiyo.

Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na kocha Bakari Shime, akisaidiwa na Sebastian Mkomwa chini ya mshauri wa ufundi wa timu za vijana Kim Poulsen, kinatarajiwa kuwa kambini kwa muda wa wiki mbili kabla ya safari kuelekea Goa India kushirki mashindano hayo.

Kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo maalumu ya vijana kimataifa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Serengeti Boys, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijanaa barani Afrika dhidi ya Shelisheli Juni 25-2 Julai, 2016.

HABARI ZAIDI

Picha ya Diddy na Cassie enzi za mahusiano yake

Diddy aomba msamaha kumshambulia EX wake Cassie

Rais wa Iran Ebrahim Raisi

Rais wa Iran afariki kwa ajali ya Helikopta

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato