John Bocco akisaini mkataba
John Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba kuanzia msimu ujao, ikiwa ni baada ya kuonesha ubora mkubwa katika msimu uliomalizika.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo, ikiwemo Twitter.
Katika msimu wa 2018/19, John Bocco ameifungia Simba mabao 16 ya ligi.