Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TFF yamwadhibu tena Nyoso

Jumanne , 13th Feb , 2018

Shirikisho la soka nchini TFF kupitia Kamati yake ya  Nidhamu imemfungia mechi tano na adhabu zingine mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mechi.

Kamati hiyo ya TFF iliyokutana Jumamosi Februari 10, 2018 pia imempiga faini ya shilingi 1,000,000 (Milioni moja) mchezaji huyo, ambapo kikao hicho kimejiridhisha kuwa Nyoso alimpiga shabiki huyo.

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo Kagera Sugar ilipoteza kwa mabao 2-0,  mabao ya Simba yakifungwa na Said Ndemla na John Bocco. Baada ya tukio hilo Nyoso alikamatwa na Polisi na kuwekwa ndani ambapo kesi yake bado inaendelea.

Nyoso amekuwa na matukio yasiyo ya kiungwana michezoni ambapo awali aliwahi kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka baada ya kumshika makalio mshambuliaji John Bocco, kipindi akiwa Azam FC huku Nyoso akiwa Mbeya City.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba

Ziara ya Rais Samia Korea kuanza rasmi Mei 31 2024

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20