Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wanafunzi wafa maji wakijifunza mkoani Geita

Jumatano , 5th Jun , 2019

Wanafunzi watatu wamefariki dunia kwa ajali ya maji baada ya baada ya Mtumbwi uliokuwa umebeba wanafunzi watano wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Makurugusi, Wilayani Chato Mkoani Geita  kupinduka eneo la Kibumba Mwaro wa Matofari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo

Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, amesema ,tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi wakati wanafunzi hao, Diana Fitina(16), Asa Gabriel(19), Mayencha Faustine(18), Masalu Hamis (22) Yohana Jamonda (19) walipofika eneo hilo kwa lengo la kufanya mafunzo kwa vitendo kuhusu Mazingira ya Ziwa Victoria.

Amesema, tukio hilo limetokea umbali wa mita 120 kutoka fukwe za Ziwa Victoria,baada ya kijana Samson Kano,aliyekuwa ndani ya mtumbwi huo  mali ya Daud Thomas,kujitosa majini kwa lengo la kuwaonyesha wenzake ujuzi wa kuogelea.

Amewataja waliokufa maji kuwa ni pamoja na Asa Gabriel, mkazi wa kijiji cha Muhororo, Manyencha Faustine na Masalu Khamis, huku Diana Fitina akilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu, baada ya kunywa maji mengi.

Aidha,tukio kama hili limewahi kutokea Mei 22, 2017 baada ya wanafunzi watatu kati ya 24 wa shule ya msingi Butwa Kata ya Izumacheli wilayani Geita, kufariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kutoka shuleni kuingiwa na maji na wao kujirusha majini na kuzama, huku  21 wakiokolewa.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava