Jumanne , 28th Mar , 2023

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amegawa mitungi ya gesi 700 kwa wanawake wajasiriamali 700 wa Mkoa wa Mwanza lengo ikiwa ni kuhamasisha kuacha matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa

Amewataka  watumie nishati safi ili kuhifadhi mazingira na pia amekabidhi fedha kiasi cha shillingi milioni 21.

Hafla hiyo imefanyika leo Machi 27, 2023 katika Ukumbi wa Rocky City Mall jijini Mwanza, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Reuben Sixbert Jichabu.

Akizungumza katika hafla hiyo, baada ya kukabidhi majiko kwa niaba ya Mhe. Masanja, Bw. Jichabu amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.

Naye, Mhe. Masanja ameahidi kuendelea kuwaunga mkono wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mwanza ili waweze kukuza uchumi wao.