Jumatatu , 26th Jun , 2023

Baadhi ya wafanyabiashara wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamesema changamoto ya uchache wa viwanda unawafanya kukosa vifungashio vya bidhaa na wengine kuvipata kwa gharama kubwa hali ambayo inaleta ushindani mkubwa sokoni kulinganisha na bidhaa zinazotoka nje.

Rai hiyo imetolewa na wafanyabiashara hao kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao wamejisajili katika maonesho ya 47 ya kimataifa yanayoanza June 28 hadi July 13 ambapo wamekutanishwa na kujadili biashara wazingatie nini kabla wakati na maonesho na baadaya ya maonesho wawe na uwezo wa kufanya tathimini.

Awali akitoa mbinu za kibiashara Mkurugenzi kutoka chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC amesema wakiwa na Bidhaa nzuri,zimefungashwa kwenye vifungashio vyenye vigezo vya ndani na kwamba kwenye maonesho ushindani ni mkubwa.

"uchache wa viwanda vinavyozalisha vifungashia unafanya wajasiriamali wengi kukwama kufunga bidhaa zao vizuri wakiingia sokoni wanakutana na ushindani mkubwa sasa maonesho kama haya tujifunze kwa wenzetu tukiiga pia teknolojia ipi wanaitumia ili nasisi tukue kibiashara haya maonesho ni kimataifa"

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema maonesho hayo kupitia banda la wafanyabiashara wanawake Tanzania imekuwa ni daraja la kuwakutanisha na viongozi wa serikali,wawekezaji kutoka nje sambamba na kuongeza ujuzi na mtandao.

Kwa mwaka huu wafanyabiashara wanawake kutoka mikoa mbali mbalimbali ya Tanzania wamepatiwa mafunzo ili kuleta ushindani kutoka kwa wawekezaji wa nje licha changamoto za vifungashio ambao bado wengi wanakabiliwa navyo katika biashara.