Jumatano , 7th Jun , 2023

Licha ya Serikali na wadau kuzidi kuweka mazingira kwa watoto wa kike kujitokeza kwa wingi katika masomo ya Sayansi bado changamoto ipo kwa baadhi ya maeneo ambapo wanawake Wahandisi Tanzania wamesema malengo yao kwa sasa kuwapa morali zaidi wasichana wenye ndoto ya kuwa wahandisi

Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi Rehana Juma ambaye ni Mwenyekiti wa wanawake wahandisi Tanzania amesema licha ya changamoto wanazopitia wasichana katika mafunzo yao lakini idadi ya wanawake wahandisi inazidi kuongezeka kila Uchwao.

Hata hivyo kwa upande wake Ester Christopher ambaye ni mhandisi mkongwe wa siku nyingi amesema umekuwa ni utaratibu wao kuandaa maonyesho ya kazi za kibunifu kutoka kwa wahandisi wanawake kutoka kwa wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wahandisi wanawake lakini pia kuwapa nafasi wahandisi wachanga ya kukutana na Magwiji kwenye sekta hiyo ya Uhandisi.

Licha ya jitihada mbalimbali ambazo serikali imekuwa ikitoa katika masomo ya sayansi kwa watoto wa kike ili kupata wahandisi wengi zaidi bado vipo baadha ya vikwazo ikiwemo kipato duni kwa baadhi ya familia na uoga.

Wanawake wahandisi kwa mwaka huu watakutana kwa siku mbili visiwani Zanzibar wakiwa na dhima ya pamoja isemayo Nguvu ya ushirikishwaji na uhusihwaji wa wanawake kwenye fani za kihandisi.