Jumapili , 20th Aug , 2017

Mzee mmoja (88) huko Kaunti ya Nyeri kijiji cha Karagoto amefariki na kuzikwa jana kwenye kaburi aliloliandaa kwa takribani miaka 30 huku akiwa ameacha sintofahamu kwa familia na majirani zake juu ya misimamo pamoja na wosia wake.

Akizungumza na chombo cha habari huko nchini Kenya jirani wa Mzee huyo amesema kuwa Marehemu kabla ya kufikwa na umauti alikuwa ameshajiandalia kaburi lake huku akiacha wosia wa kutozikwa sehemu nyingine yoyote zaidi ya kwenye kaburi alilolijenga kwa miaka 30 pia kuktaka kutopelekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti.

Kwa mujibu wa jirani  huyo alimtaja Mzee huyo aliyefahamika kwa jina la Mwendazake Stanley Muryuki kwamba alikuwa ni mtu aliyesimamia misimamo yake hata baada ya kuumwa kwa muda mrefu hakutaka kwenda hospitali kwa madai kuwa Mungu afabnye apendavyo juu yake lakini siyo kupelekwa hospitali.

Mwendazake ambaye alikuwa muumini mzuri wa dhehebu la Katoliki aliacha wosia kwa familia yake kuwa endapo atafariki waombolezaji wote wapatiwe sahani ya chakula kabla ya kuondoka huku akiomba Padri aongoze mazishi yake na vijana wake wamlinde kwa muda usiopungua saa 24.