Jumanne , 19th Oct , 2021

Kijana Sooraj Kumar (28) kutoka Kerala nchini India amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumuuwa mkewe Uthra (25) Mei 2020 kwa kutumia sumu kali ya nyoka anayejukana kama Cobra.

Picha ya Sooraj Kumar akiwa Mahakani

Waendesha mashtaka wamesema Kumar, ambaye alikuwa mfanyakazi wa benki, hakuwa na furaha katika ndoa yake na aliogopa kutoa talaka kwa Uthra kwasabau angelazimika kurudisha mahari kubwa, gari mpya na takriban dola 20,000 ambazo ni zaidi ya Tsh. Milioni 46.