Alhamisi , 19th Jan , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewateua Mabalozi watano kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

Balozi Dkt. Emmanuel nchimbi

 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Mabalozi walioteuliwa na vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo;

  1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Beijing – China.
  2. Balozi George Kahema Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
  3. Balozi Emmanuel John Nchimbi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
  4. Balozi Fatma M. Rajab ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha- Qatar.
  5. Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
  6. Balozi Dkt. James Alex Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.

Mabalozi hawa wataapishwa kesho tarehe 20 Januari, 2017 saa 10:30 Jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi.

Tarehe ya kuapishwa na kituo cha kazi cha Bw. Muhidin Ally Mboweto kitatangazwa baadaye.