Jakaya Kikwete achukizwa

Tuesday , 19th Sep , 2017

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amefunguka na kuonyesha kuchukizwa na taarifa za uzushi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuhusu yeye akionekana kujibu moja ya kauli ya Rais John Pombe Magufuli jambo ambalo si la kweli.

Kikwete ametumia mtandao wake wa twitter kuonyesha masikitiko yake hayo kwa watu wanaofanya jambo hilo huku akionyesha kusikitishwa zaidi na mapokeo ya watu ambao wengi wao wameiamini hiyo kauli wakidhani huenda ni kweli imetoka kwake kitu ambacho si cha kweli. 

"Nasikitishwa sana na uvumi huu unaosambazwa juu yangu. Inasikitisha sana. Inasikitisha zaidi kuwa wako watu timamu wanaoamini uzushi huu" alisema Jakaya Kikwete 

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyu mstaafu kuzushiwa uzushi na watu kupitia katika mitandao ya kijamii