Jumatatu , 18th Sep , 2017

Kimbunga kikali na chenye nguvu kubwa kimetokea magharibi mwa Romania na kuuwa watu wanane pia kujeruhi wengine zaidi ya 67, kwa mujibu mwa maafisa wa eneo hilo.

Wengi wa waliothiriwa walikuwa ndani na nje ya mji wa Timisoara ambapo upepo ulifika kasi ya kilomita 100 kwa saa na ulioangusha miti na kuong'oa paa za nyumba jambo ambalo limepelekea baadhi ya huduma za umeme na maji kukatwa.

Meya wa mji wa Timisoara Nicolae Robu amezungumza na kusema, "Hatukuonywa kuhusu hili, ripoti ya hali ya hewa ilisema kuwa kungekwa na mvua na sio kimbunga kama hiki, kama tungejua kuhusu hili basi tungejiandaa kukabiliana nalo". 

Taasisi za huduma za dharura nchini Romania zimewashauri watu kubakia majumbani mwao na kuacha kwenda karibu na miti na nyaya za umeme.

Baada ya Kimbunga hicho kuharibu eneo hili, kwa sasa kinaelekea kaskazini kwenda Ukrain.