Jumapili , 20th Aug , 2017

Gavana mteule wa jimbo la Nairobi nchini Kenya Mike Sonko, ameingia kitendo cha Rais Magufuli alichofanya baada ya kuingia madarakani cha kuingia mtaani na kufanya usafi, huku akiweka kampeni maalum ya usafi.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Mike Sonko ameweka picha na kuandika kuwa serikali yake itasimima suala hilo ili kuweka mji safi, ili kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya kumbukiza.

“Ni muhimu kwetu kujua na kuweka mazingira safi  kwani muhimu kwa maisha yetu, na serikali yangu itawezesha kila kinachohitajika ili kufanya usafi, ili kuonyesha dhamira yetu tumetoa  mapipa ya kutunzia takataka 20, mikokoteni 10, koleo 10, reki 10, viatu, mipira ya mikono  na vitu vingine kwa kila kata hapa Nairobi,  kwa kazi za kawaida:”, aliandika Sonko.

Sonko aliendelea kuandika “Tukitaka kuondokana na kipindu pindu a magonjwa mengine mabaya, tunahitaji kuweka mazingira yetu safi, nahimiza kuacha kutupa taka hovyo, tutumie hivi vifaa ipasavyo na kuhakikisha tunasafisha makazi yetu”, aliandika Sonko.

Mike Sonko aliendelea kusema kuwa wakifanikisha hilo wataweza kuepukana pia na mafuriko, na kuwataka watu wa Nairobi kuwa mawakala wa usafi.

Alichopost Mike Sonko Instagram
Rais John Magufuli wa Tanzania akifanya usafi.