Jumapili , 25th Sep , 2016

Wilaya ya Monduli imefanikiwa kupunguza ajali za barabarani za pikipiki kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi mwezi wa nane kupitia kampeni maalum ya mafunzo ya sheria ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Munduli Idd Kimanta wakati akifunga mafunzo ya kuhusu sheria za usalama barabarini kwa madereva pikipiki, na kuwataka madereva hao kupitia kazi yao kulinda na kuitunda amani iliyopo ili kuongeza kipato chao.

Baadhi ya madereva bodaboda wamesema kuwa mahusiano hafifu kati yao na jeshi la polisi yametokana na ukosefu wa elimu hivyo kupitia mafunzo hayo watashiriki kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kuchangia kodi .

Naye Mkurugenzi wa Apec, Respicus Timanya ambao ndio waratibu wa mafunzo hayo, ameiomba serikali kuwasamehe madeni makumbwa ya kodi wamiliki wa bodaboda ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawachangi kodi na badala yake kuanza kupunguza madeni yao, ili kutoa nafasi kwa wamiliki wa bodaboda waanze kulipa kodi.

Zoezi hili la utoaji mafunzo limefanyika katika wilaya ya Arumeru na Monduli ambapo zaidi ya waendesha bodaboda 250 wameshiriki.