Ijumaa , 20th Oct , 2017

Mwanamuziki wa Afrika Kusini ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge nchini humo, Jennifer Ferguson, amesema hataki kumshtaki mtu aliyembaka kwani hana imani na mfumo wa mahakama wa nchi hiyo.

Akifanya mahojiano na BBC Jennifer ambaye kwa sasa anaishi Sweden, amesema haamini kabisa na utendaji wa mahakama nchini Afrika Kusini, na kufungua kesi hiyo itakuwa ni sawa na kutonesha vidonda vibichi.

Jennifer ambaye aliweka wazi kuwa alibakwa na kuumizwa na mnamo mwaka 1993, na Danny Jordaan katika chumba cha hoteli kwenye mji wa Elizabeth, na mpaka sasa hajafanya uamuzi wa kumshtaki mtu huyo, ingawa aliamua kuzungumza juu ya tukio hilo kutekeleza kampeni ya kuvunja ukimya kwa wanawake wanaonyanyasika kijinsia.

Danny Jordaan ambaye ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu na pia Meya wa mji mmoja huko nchini Afrika Kusini, hajawahi kujibu chochote dhidi ya tuhuma hizo za kumbaka binti huyo.

Serikali ya Afrika Kusini imesema kwenye mwaka wa fedha uliopita takriban kesi 4,600 zilifunguliwa,huku watafiti wakisema idadi hiyo ni ndogo sana kwani kuna matukio mengi ya ubakaji ambayo hayaripotiwi.

 

Jennifer Ferguson ambaye alibakwa