Serikali yatoa onyo kali

Tuesday , 19th Sep , 2017

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Fortunatus Musilimu, ameahidi kuwachukulia hatua kali wavunjifu wote wa sheria za usalama barabarani pasipo kujali nyadhifa, madaraka na umaarufu wa mtu husika katika jamii.

ACP Musilimu ametoa onyo hilo jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshiriki shindano la uelewa wa sheria za barabarani kupitia michoro mbali mbali, shindano lililoandaliwa na Kampuni ya mafuta ya Puma Energy ambamo serikali inaumilikia wa asilimia hamsini.

Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Bw. Philippe Corsaletti amesema shindano hilo pamoja na programu nyingine za usalama barabarani zinazofadhiliwa na kampuni hiyo zinalenga kujenga kizazi kitakachokuwa na uelewa wa juu kuhusu usalama barabarani ili kulinda nguvu kazi ya taifa inayohitajika katika uzalishaji.