Jumatano , 20th Apr , 2016

Kituo cha EATV leo kimethibitisha rasmi kwamba kitaanza kurusha tamthilia kali inayokwenda kwa jina la 'Siri za Familia' kwa lengo la kuwapa watazamaji fursa ya kupata uhalisia wa maisha.

Mwigizaji wa tamthilia ya 'Siri za Familia' Dayana William alipokuwa akielezea maudhui ya tamthilia hiyo kwa waandishi wa habari hawapo pichani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Vipindi vya EATV Bi. Lidya Igarabuza amesema EATV imekubali kurusha tamthilia hiyo kwa lengo la kuinua vipaji vya nyumbani na ikizingatiwa kwamba lengo kubwa la EATV ni kuonyesha vipindi vingi vinavyozalishwa kwa maudhui ya hapa nchini yanayoigusa jamii moja kwa moja.

Kwa upande wahusika katika tamthilia hiyo 'Characters' wameishukuru EATV kwa kukubali kuonyesha watu kazi zao na kwamba kwa kufanya hivyo kunatoa fursa kwao kuonesha vipaji vyao na kutoa ujumbe wenye maadili ya kitanzania.

Tamthilia hii itaonyeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu mfulilizo kila siku ya jumatatu hadi alihamisi saa 12:30 jioni hadi saa moja 7:00 jioni.

Baadhi ya wahusika hao ambao wameipika tamthilia hiyo ni pamoja na Dayana William (Princes) kwenye tamthilia ataonekana kama binti ambaye akiona mtu mwenye pesa macho yote yanaelekea huko na atakua funzo kwa wadada kutokana na uhalisia atakaouonesha.

Kojak Chilo (Shaka Zulu) ataigiza kama baba wa familia ambaye ni makini katika kujenga familia na kuonesha ukomavu katika utendaji wa kazi za familia.

Mrisho Salehe Zimbwe (Kalos) Ndiye muhusika mkuu katika tamthilia hii ambaye ataonyesha namna siri za familia zinavyokuwa katika jamii yetu ndiye ataunganisha matukio mbalimbali.

Abdul Thomson Yeye ataigiza kama tajiri sana, Jacklin Gabriel ataigiza kama mwanamke jeuri sana ambaye ni mgomvi na na ana msimamo katika mambo yake.

Aidha Watazamaji wote wameombwa kutizama tamthilia hiyo na ambao watakosa muda watatazama marudio ambayo yatatangazwa na kituo kwa lengo la kupata ujumbe mahususi uliopo kwenye tamthilia hii.