Jumatatu , 18th Sep , 2017

Serikali imefanikiwa kumaliza tatizo la maji safi na salama eneo la Kilungule B Kimara Jijini Dar es salaam,eneo ambalo halikua na huduma hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza leo mara baada ya kuzindua kizimba jamii cha maji safi kilichotengenezwa na shirika la maji safi na maji taka DAWASCO kupitia fedha zilizotolewa na serikali kuu Mkuu wa wilaya ya Ubungo Kisare Makore amesema maendeleo hayo yanayofanywa na serikali ni jukumu la kila mwana jamii kuhakikisha wanasimamia uzalishaji wa huduma hiyo ili kupunguza kero za maji.

Kwa upande wake meneja wa DAWASCO kwa eneo la Kimara Injinia Pascal Fumbuka amesema utekelezaji wa mradi huo ni wa kilomita nne na unatarajia kuhudumia wanachi zaidi ya elfu 5000 katika eneo hilo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimara Pascal Manota amesema wanafanya jitihada za kuhakikisha maji hayo yanawanufaisha wanachi wa eneo hilo na jirani kwakuwa kwa kipindi cha nyuma yameripotiwa matukio mengi ya watu kuumia pindi wanapoenda kutafuta maji safi.